Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kaisari Wilhelm I (Berlin, 22 Machi 1797 - Berlin 9 Machi 1888) alikuwa mfalme wa Prussia kuanzia mwaka 1861 na kuanzia mwaka 1871 kaisari wa Ujerumani. Alizaliwa kwa jina la Wilhelm Friedrich Ludwig von Preußen. Babake alikuwa mfalme Friedrich Wilhelm III wa Prussia.
Tangu utoto alilelewa kama mwanajeshi akapewa cheo cha kijeshi kwa umri wa miaka 9. Mwaka 1814 alipokuwa na miaka 17 aliamrisha kikosi cha wanajeshi katika vita dhidi ya Napoleoni. Mwaka 1829 alimwoa Augusta binti wa mtemi wa Sachsen-Weimar-Eisenach wakapata watoto wawili na mwanawe Friedrich alimfuata baadaye kama mfalme na kaisari.
Baada ya kifo cha baba mwaka 1840 kakaye Friedrich Wilhelm IV alikuwa mfalme na Wilhelm alipewa cheo cha malme mteule.
Wakati wa mapinduzi ya Ujerumani ya 1848-49 alikuwa kiongozi wa kijeshi aliyekandamiza wapiganaji wa demokrasia katika sehemu malimbali.
Kutokana na ugonjwa wa mfalme alianza kutawala Prussia tangu 1857 na baada ya kifo cha kaka alipokea taji la mfalme tarehe 2 Januari 1861. Mwanzoni alipendelea siasa ya upatanisho na bunge la Prussia lakini lilipokataa kumpa pesa kwa ajili ya jeshi jinsi alivyotaka aliachisha serikale yake na kumpa Otto von Bismarck madaraka ya waziri mkuu. Pamoja na Bismarck alifuata mipango yake ya kijeshi hata bila kibali cha bunge.
Bismarck alimshauri mfalme na kumwongoza katika hatua tatu ziliokuwa kwa maendeleo ya Ujerumani kwanza vita dhidi ya Austria, pili vita dhidi ya Ufaransa na umoja wa Ujerumani na tatu sheria za wafanyakazi zilizoanzisha muundo wa bima kwa wote uliopo hadi leo nchini Ujerumani.
Kwa vita dhidi ya Austria ya 1866 Wilhelm na Bismarck waliondoa Austria kutoka mashindano ya Uongozi wa Ujerumani na kupeleka Prussia mbele.
Kwa vita dhidi ya Ufaransa ya 1870-71 waliunganisha madola madogo ya Ujerumani na kuunda Dola la Ujerumani. Hadi mwisho Wilhelm alipinga kuanzishwa kwa cheo cha Kaisari ya Ujerumani alipendelea kuwa mfalme wa Prussia pekee. Lakini hata katika swali hili Bismarck alishinda na tarehe 18 Januari 1871 Wilhelm alitangazwa kuwa Kaisari wa Ujerumani na mkuu wa Dola la Ujerumani jipya.
Pamoja na Bismrck na kulingana na umri mkubwa chini ya uongozi wa chansella huyu aliendelea kutawala hadi kifo chake mwaka 1888.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.