From Wikipedia, the free encyclopedia
Ignas wa Antiokia (kwa Kigiriki Ἰγνάτιος, Ignatios; alijulikana pia kwa jina la Θεοφόρος, Theophoros, yaani "Mleta Mungu"; 35/50 B.K. - 98/117[1]).
Ni kati ya Mababu wa Kanisa wa kwanza, akiwa mwanafunzi wa Mtume Yohane na askofu wa tatu wa Antiokia, leo nchini Uturuki.
Chini ya kaisari Traiano, alihukumiwa kuliwa na wanyamapori, na kwa ajili hiyo alifikishwa Roma alipofia dini yake: safarini, huku akionja ukatili wa walinzi wake, alioufananisha na ule wa chui, aliandika barua kwa makanisa mbalimbali na kwa Polikarp Mtakatifu , alimohimiza ndugu zake katika imani kumtumikia Mungu katika ushirika na maaskofu na wasimzuie kuchinjwa sadaka kwa Kristo[2].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake inaadhimishwa na Wakatoliki[3][4], Waanglikana na Waorthodoksi wa Mashariki kwenye 17 Oktoba, lakini na Waorthodoksi tarehe 20 Desemba.
Kati ya barua zake, zimetufikia saba za hakika ambazo ni kama kielelezo cha teolojia ya awali ya Ukristo. Humo kwa mara ya kwanza tunasoma juu ya Kanisa Katoliki ambalo linaitwa hivi kwa kulitofautisha na makundi ya Wakristo waliotengana nalo.
Kati ya mada muhimu zaidi kuna Kanisa, sakramenti na nafasi ya askofu pekee katika kila jimbo.
Barua zake zimetafsiriwa kwa Kiswahili na kutolewa Italia kama ifuatavyo: MT. IGNASI WA ANTIOKIA, Nyaraka - tafsiri ya B. Santopadre n.k. – ed. E.M.I. – Bologna 1992 – ISBN 88-307-0404-0
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.