From Wikipedia, the free encyclopedia
Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia (International Atomic Energy Agency (IAEA)) ni mamlaka ya kujitawala ya kimataifa inayoshirikiana na Umoja wa Mataifa (UM). Ilianzishwa tar. 29 Julai 1957 na nchi 81 wanachama wa UM.
Hata kama si moja kwa moja chini ya katiba ya UM inatoa taarifa zake kwa Mkutano Mkuu wa UM na Baraza la Usalama la UM.
Shabaha ya IAEA imekuwa tangu mwanzo matumizi ya nishati ya nyuklia yanayolingana na amani. Hapa imepewa madaraka ya kuangalia vituo vya kinyuklia katika nchi zote, kusaidia upanuzi wa teknolojia ya kinyuklia isiyo ya kijeshi na usalama wa matumizi ya nishati ya nyuklia. Shabaha muhimu ni pamoja na kuzuia uenezaji wa silaha za nyuklia.
IAEA ni shirika la kimataifa linalopaswa kuangalia masharti ya mkataba wa kuzuia usambazaji wa silaha za nyuklia wa 1968.
IAEA ina mikono mitatu:
Kazi inatekelezwa katika idara sita za utawala, sayansi ya nyuklia na matumizi yake, nishati nyuklia, usalama wa nyuklia, ushirikiano wa kiteknolojia na usimamizi wa vituo vya kinyuklia duniani.
Makao makuu yapo kwenye Jiji la UM huko Vienna (Austria). Ofisi za kanda zipo Toronto and Tokyo, halafu kuna ofisi ndogo kwenye makao ya UM huko New York na Geneva. IAEA ina pia maabara ya uchunguzi katika Seibersdorf (Austria) na Monako.
Udhaifu mmojawapo wa IAEA ni katiba ya kwanza inayodai kibali cha nchi wanachama kwa uchunguzi wa hali ya vituo vya nyuklia katika nchi hizi. Kwa njia hii nchi kadhaa ziliweza kuficha jitihadi zao za kuunda silaha za kinyuklia. Kwa sababu hiyo kuna mapatano mapya inayoruhusu wachunguzi wa IAEA kuingia katika maabara na taasisi ziote zinazoshughulikia mambo ya nyuklia wakati wowote. Ila tu haya mapatano mapya yalikubaliwa na nchi 73 pekee hadi 2006.
IAEA pamoja na mkurugenzi Mohamed ElBaradei ilipokea tuzo ya Nobel ya Amani mwaka 2005. Tuzo hili lilitolewa kwa sababu IAEA ilijitahidi kuzuia uvamizi wa Irak mwaka 2001.
Wataalamu wa UM walikuwa wametambua maabara ya kinyuklia nchini Irak yaliyofichwa kinyume na masharti ya mkataba wa kuzuia usambazaji wa silaha za nyuklia. Katika miaka kabla ya uvamizi wa Irak na Marekani IAEA ilifaulu kuchunguza maabara na ofisi nyingi hadi Irak haikuwa tena na utafiti wa kuunda silaha za nyuklia isipokuwa serikali ya Marekani haikuamini taarifa za IAEA na kushambulia Irak hata hivyo. Kamati ya Nobel iliamua ya kwamba IAEA ilijitahidi kuzuia matumizi ya kijeshi ya nishati ya nyuklia na kujenga matumizi salama ya nishati hii.
Tovuti rasmi ya IAEA Archived 25 Oktoba 2012 at the Wayback Machine.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.