From Wikipedia, the free encyclopedia
Harun ar-Rashid (kwa Kiarabu هارون الرشيد) alikuwa khalifa wa tano wa nasaba ya Waabbasi aliyetawala milki kubwa ya Kiislamu (zaidi ya Iran, Iraq, Saudi Arabia, Syria na Afrika Kaskazini) kati ya miaka 786 hadi 809 BK.
Alizaliwa mjini Ray (Uajemi) akafariki mjini Tus (Uajemi) wakati wa vita dhidi ya waasi.
Kipindi chake cha utawala kilikuwa na maendeleo makubwa ya elimu na utamaduni. Sanaa ya Kiislamu (ikiwa pamoja na muziki) ilistawi.
Maktaba yake ilikuwa msingi kwa taasisi ya Nyumba ya hekima (Dar-al-Hikma) mjini Baghdad iliyokuwa kama chuo kikuu ambako vitabu vingi vilitafsiriwa kwa lugha ya Kiarabu kutoka Kigiriki, Kichina, Kisanskrit, Kiajemi na Kiaramu (Syriac). Kwa njia hiyo Baghdad ilikuwa kitovu cha elimu cha kimataifa wakati huo.
Harun alituma mabalozi kwenda hadi China na pia kwa Kaisari Karolo Mkuu wa Dola Takatifu la Kiroma.
Mwaka 796 Harun ar-Rashid alihamisha mji mkuu wake kutoka Baghdad kwenda Raqqa katika Syria.
Anakumbukwa kama mtu wa hekima kubwa, akionekana hivyo katika hadithi za Alfu Lela U Lela.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.