Guruguru (familia)
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Guruguru ni mijusi wa familia Gerrhosauridae walio na magamba magumu mgongoni. Mbavuni wana kunyanzi la ngozi kwa urefu mzima wa mwili.
Guruguru | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Guruguru koo-njano (Gerrhosaurus flavigularis) | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Nusufamilia 2, jenasi 7:
| ||||||||||||||||
Mwongoni mwa mijusi hawa kuna spishi kubwa kabisa za Afrika: hadi sm 75. Lakini nyingi ni sm 30-45. Mkia wa spishi za guruguru-nyoka (Tetradactylus) ni mrefu sana, zaidi ya mara mbili ya urefu wa mwili. Na miguu yao ni mifupi au haipo.
Huishi kati ya mawe na miamba, katika vishimo, katika vichuguu au takataka ya majani na matawi. Chakula chao ni wadudu hasa, kama panzi, mchwa na sisimizi, lakini majongoo, tandu, konokono na mijusi wengine pia, na spishi nyingine hula matunda na maua pia.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Guruguru (familia) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.