From Wikipedia, the free encyclopedia
Gneis (pia "gneiss") ni aina ya mwamba metamofia inayopatikana kwa wingi duniani. Asili yake ni miamba mashapo (sedimentary rocks) na pia miamba ya mgando (igneous rocks) iliyoathiriwa na joto pamoja na shinikizo kubwa kwa miaka mingi.[1]
Jina la gneis / gneiss lina asili ya Kijerumani ambapo inamaanisha kitu kinachong'aa, maana wakati mwingine kuna fuwele vimeto ndani yake[2].
Miamba ya gneis kwa kawaida huonekana kuwa na milia ya madini yenye rangi tofauti. Ilitokea katika vilindi vya ardhi ambako ilishinikizwa na uzito mkubwa wa miamba juu yake. Katika hali hiyo mwamba si imara lakini kinamo. Miendo katika ganda la dunia huvuta na kusukuma mwamba kinamo na hapo madini ndani ya mwamba huanza kuachana kiasi na kuganda tena kwa matabaka ya pekee yanayoonekana kama milia ya gneis[3].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.