Ethanoli (pia: alkoholi ethili) ni dawa lililopo ndani ya aina zote za vinywaji vya pombe.

Thumb
Muundo wa kikemia wa ethanoli. C ni kaboni, H ni hidrojeni na O ni oksijeni.
Thumb
Molekuli ya ethanoli (hidrojeni ni nyeupa, kaboni ni kijivu na oksijeni nyekundu)
Thumb
A bottle of Ethanol

Kikemia ni kampaundi ogania inayopatikana kama kiowevu kisicho na rangi. Ikiwa ni dawa safi inawaka haraka lakini mara nyingi hupatikana kama mchanganyiko pamoja na maji katika aina za pombe; hapa inawaka tu kama asilimia yake inapita kiwago cha 60%.

Fomula yake ni C2H5OH inayoandikwa pia C2H6O. Ni dawa lenye tabia ya sumu kiasi kwa mwili wa kibinadamu pia ina tabia ya kuyeyusha.

Ethanoli kama fueli

Ethanoli ina pia matumzi ya fueli badala ya petroli. Inawaka ndani ya injini ama peke yake au ndani ya mchanganyiko wa petroli na ethanoli.

Nchini Brazil ethanoli hutengenezwa kwa wingi kutokana na miwa na sasa inatosheleza asilimia 18 ya mahitaji ya fueli ya magari katika nchi hii. [1] Watu wengine wanaona tatizo katika teknolojia hii maana mashamba makubwa yanatumiwa kwa miwa hayapatiokani tena kwa vyakula na maeneo makubwa ya misitu asilia yametumiwa pia..

Marejeo

Viungo vya Nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.