From Wikipedia, the free encyclopedia
Dunstan wa Canterbury (909 – 19 Mei 988)[1] alikuwa abati wa Glastonbury Abbey, halafu askofu wa Worcester, London, na hatimaye askofu mkuu wa Canterbury[2], mbali ya kuwa waziri chini ya wafalme kadhaa.
Kwa juhudi zake alirekebisha, alipatanisha na kueneza umonaki na Kanisa la Uingereza kwa jumla.
Osbern wa Canterbury, aliyeandika maisha yake katika karne ya 11, alisifu uwezo wake katika uandishi na uchoraji.[3]
Tangu kale aliheshimiwa kama mtakatifu, jambo lililothibitishwa na sinodi ya Winchester ya mwaka 1029.
Wakatoliki[4], Waorthodoksi[5] na Waanglikana wanaadhimisha sikukuu yake tarehe ya kifo chake.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.