From Wikipedia, the free encyclopedia
Dekkani (kwa Kiingereza: Deccan) ni tambarare kubwa ya juu inayojumisha sehemu kubwa ya Uhindi Kusini.
Tambarare hii inaenea katika majimbo manane ya Uhindi (Telangana, Maharashtra, Andhra Pradesh, Karnataka, Kerala na Kitamil Nadu).
Maeneo yake kwa jumla ni zaidi ya km² 422,000 ambazo ni sawa na asilimia 43 za Uhindi wote.[1]
Umbo la Dekkani ni takriban kama pembetatu; kwa pande mbili kuna bahari na upande wa kaskazini Bara Hindi inaendelea kwenye nchi kavu. Upande wa magharibi milima ya Ghat ya Magharibi inatenga tambarare ya juu na bahari, upande wa mashariki ni safu ya Ghat ya Mashariki. Sehemu hizi za milima huinuka kutoka katika nchi tambarare za pwani hukutana katika ncha ya kusini ya Uhindi. Mpaka wa kaskazini wa pembetatu unafanywa na milima ya Satpura na milima ya Vindhya. Milima hiyo hutenganisha Dekkani na watu wake na kaskazini ya nchi.
Asili ya jina "dekkani" iko katika neno la kienyeji linalomaanisha "kusini" [2] [3]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.