From Wikipedia, the free encyclopedia
Hifadhi ya Comoé ni hifadhi ya bioanwai iliyoandikishwa katika orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia nchini Cote d'Ivoire. Ni hifadhi kubwa zaidi inayolindwa huko Afrika Magharibi, ikiwa na eneo la km2 11,500. Upande wa kusini inaanza katika sehemu yenye mchanganyiko wa savana na misitu ikiendelea hadi maeneo yabisi ya kaskazini.[1]
Comoé National Park | |
IUCN Jamii II (Hifadhi ya Taifa) | |
Ramani ya mto Comoe katika Cote d'Ivoire, hifadhi iko kaskazini kabisa | |
Mahali | Côte d'Ivoire |
---|---|
Eneo | km2 11 500 (sq mi 4 400) |
Kuanzishwa | 1983 |
Kando ya Mto Comoé kuna bado sehemu za misitu ya mvua ya kitropiki ambayo kawaida hupatikana kusini tu. [2]
Mazingira ya hifadhi ya Comoé yalikuwa na wakazi wachache tangu kale kutokana na ardhi isiyo na rutuba, kupatikana kwa upofu wa mto kwenye mito na wingi wa mbu wa mbung'o wanaoeneza ugonjwa wa malale pamoja na nagana ya mifugo[3][4].
Wakoloni Wafaransa walitenga maeneo baina ya mito Comoe na Boua kuwa hifadhi ya wanyama. Hifadhi hiyo ilipanuliwa baada ya uhuru.
Hifadhi hiyo inafanywa hasa na tambarare zilizopitiwa na Mto Comoé pamoja na matawimito yake (mto Iringou, mto Bavé, mto Kongo).
Kuna pia madimbwi mbalimbali ya kudumu pamoja na mengine yanayokauka wakati wa kiangazi.
Ardhi ni kwa sehemu kubwa duni na haifai kwa kilimo. Milima midogo kadhaa inainuka hadi mita 600 juu ya uwiano wa eneo ambalo kwa kawaidi liko mita 120-500 juu ya usawa wa bahari.[1]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.