From Wikipedia, the free encyclopedia
Muungo kemia (kwa Kiingereza: chemical bond) ni kani inayoshikiza atomu, ioni na molekuli na hivyo kuwa msingi wa kutokea kwa kampaundi.
Kani hiyo inaweza kutokana na kani umemetuamo (electrostatic force) katika muungo ionia au na muungo kovalensi ambapo atomu zinashirikiana elektroni.
Muungo ionia unashikiza atomu zake, zinazopatikana kwa umbo la ioni, kutokana na tofauti ya chaji za ioni. Hutokea hasa kwenye chumvi mbalimbali yaani kampaundi za metali na simetali zinazopangwa kwa muundo wa fuwele.
Elementi simetali zinafanya muungo kwa kushirikiana elektroni kwenye mzingo elektroni wa nje. Atomu zinaelekea kufikia hali ambapo mzingo elektroni wa nje unajaa nafasi zote zinazowezekana. Mfano: atomu sahili ya hidrojeni ina mzingo mmoja wenye elektroni moja tu. Hii ni sababu ya kwamba atomu yake inaungana kirahisi na atomu nyingine ya hidrojeni kuwa molekuli ambapo atomu mbili za hidrojeni zinashirikiana elektroni zake na hivyo kufikia idadi ya juu inayowezekana katika mzingo wa ndani, yaani elektroni mbili. Vivyo hivyo hidrojeni inaungana kirahisi na elementi tofauti ambazo ziko tayari kupokea elektroni yake kwa kukamilisha mzingo wa nje.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Muungo kemia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.