Bustani ya Zanzibar From Wikipedia, the free encyclopedia
Bustani za Forodhani (pia hujulikana kwa Kiingereza kama Forodhani Gardens, Jubilee Gardens na zaidi hivi karibuni kama Forodhani Park)[1] ni bustani ndogo kwenye Mji Mkongwe wa Zanzibar, Tanzania.
Bustani hizo ziko kando ya mtaa wa Mizingani unaopita ukingo wa bahari wa Mji Mkongwe, mbele tu ya majengo ya Jumba la Maajabu (House of Wonders) na Ngome Kongwe (Old Fort). Bustani hiyo ilianzishwa mwaka 1936 na kufunguliwa rasmi tarehe 21 Desemba 1936 kwa maadhimisho ya jubilii ya miaka 25 za utawala wa Sultani Khalifa bin Harub wa Zanzibar (silver jubilee) na pia kwa heshima ya marehemu mfalme George V wa Uingereza aliyewahi kutimiza miaka 25 ya utawala kwenye mwaka 1935[2]. Ilijulikana kama Jubilee Gardens ikabadilshwa jina baada ya mapinduzi ya Zanzibar ya 1964[3].
Bustani zina shughuli nyingi haswa baada ya jua kuchwa, wakati watalii na wenyeji vilevile hukusanyika kwenye soko maarufu la barabara la chakula katika uwanja mkuu, kula chakula cha jioni wakifurahia vyakula vitamu vya Waswahili na Wazanzibar kama vile dagaa wa baharini, samamo, mihogo na viazi vitamu.[4] Mnamo 31 Julai 2009, hafla ya kuvunja ardhi ilifanywa na Aga Khan kuanzisha bustani iliyofufuliwa. Ilirekebishwa na Agha Khan Trust for Culture (AKTC) kwa gharama ya $ milioni 3 (Shilingi bilioni 3.9) kutoka kwa makadirio ya awali ya $ milioni 2.4 (zaidi ya Shilingi bilioni 3).
Ukarabati huo wa juu ulihusisha urejeshwaji wa barabara za waenda kwa miguu, mandhari, uboreshaji wa miundombinu, ikijumuisha taa, mifereji ya taka na vifaa vya uraia, na ukarabati wa ukuta wa bahari ulio mbele ya bustani.[5]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.