From Wikipedia, the free encyclopedia
Mlangobahari wa Bering (kwa Kirusi: Берингов пролив; kwa Kiingereza: Bering Strait) ni mlango wa bahari na mahali pa kukaribiana kati ya Alaska upande wa Amerika ya Kaskazini na Siberia upande wa Asia.
Mlangobahari wa Bering una upana wa takriban kilomita 92 na kina cha mita 30 hadi 50 pekee. Unaunganisha bahari ya Aktiki na Pasifiki.
Jina limetokana na Vitus Bering aliyekuwa Mdenmark katika utumishi wa Urusi aliyevuka mlangobahari huo mwaka 1728.
Kando ya mlangobahari wa Bering pande zote mbili maeneo yana watu wachache kwa sababu ya mazingira ya baridi.
Kufuatana na nadharia za wataalamu wa historia hapa palikuwa mahali pa kuvuka kwa watu wa kwanza kutoka Asia kwenda Amerika. Inafikiriwa ya kwamba wakati wa Enzi ya Barafu miaka 10,000 iliyopita kiasi kikubwa cha maji duniani kilipatikana kwa umbo la barafu na hivyo kiasi cha maji kiowevu kilikuwa kidogo kuliko leo. Kwa sababu hiyo usawa wa bahari ulikuwa takriban mita 121 chini ya uwiano wa leo[1] na mlangobahari wa Bering ulikuwa mkavu ukapitika kwa miguu. Hivyo watu waliingia kwa mara ya kwanza barani Amerika.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.