Bahari ya Kusini (pia: Bahari ya Antaktiki) ni jina jipya katika jiografia. Linamaanisha maji yote ya kusini ya latitudo ya 60 yanayozunguka bara la Antaktiki.

Thumb
Bahari ya Kuini inayozunguka bara la Antaktiki.
Thumb
Ramani hii inaonyesha mabadiliko ya halijoto ya maji ya bahari za dunia katika mwendo wa mwaka. Inaonekana jinsi gani kanda la barafu linalozunguka pwani la Antaktika (chini kabisa, rangi ya kijivu) hupanuka na kurudi nyuma kila mwaka.

Katika eneo hilo maji ya Bahari ya Atlantiki, Bahari Hindi na Pasifiki hukutana na kuingiliana. Kwa muda mrefu wataalamu wa Shirika la Kimataifa la Hidrografia walihesabu eneo kama vitengo vya kusini vya bahari hizo tatu kubwa lakini katika karne ya 20 wazo la kuitazama kama bahari ya pekee imesambaa na Bahari ya Kusini imerudi kwenye ramani. [1]

Eneo lote ni la kilomita za mraba 20,327,000 za maji. Linazunguka pwani ya Antaktiki yenye urefu wa kilomita 17,968. Kina kirefu ni mita 5,805 hivi.

Sehemu zake karibu na pwani hufunikwa na barafu inayokua wakati wa baridi. Katika miezi ya joto vipande vikubwa vya barafu humeguka na kuelea katika maji kama siwa barafu ambayo ni hatari kwa meli lakini zinayeyuka polepole kadiri zinavyofikia maji yasiyo baridi.

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.