From Wikipedia, the free encyclopedia
Aureliano wa Arles (523 – 551) alikuwa Askofu mkuu wa Arles (Ufaransa) miaka 546 - 551.[1]
Baba yake, Saserdosi wa Lyon, alipata kuwa Askofu mkuu wa Lyon akafariki 552.
Aureliano alifanywa na Papa Vijili kuwa balozi wake kwa Gallia yote akaanzisha monasteri mbili huko Arles, moja ya wanaume, ya pili ya wanawake, akaandika kanuni mbili mpya.[2][3][4][5][6][7]
Alifariki Lyon tarehe 16 Juni 551.[8]
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake, 16 Juni[9][10].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.