Augustino wa Canterbury

From Wikipedia, the free encyclopedia

Augustino wa Canterbury

Augustino wa Canterbury (kwa Kilatini Augustinus Cantiacorum) alizaliwa Roma, Italia, 13 Novemba 534 akafariki Canterbury, Uingereza, 26 Mei 604) alikuwa mmonaki kutoka Italia aliyetumwa na Papa Gregori I kama askofu mmisionari huko Uingereza mwaka 597 akiwa na wamonaki wenzake wengi.

Thumb
Augustino wa Canterbury katika mavazi ya Askofu mkuu.

Baada ya kupokewa vizuri na mfalme Ethelbert wa Kent, aliiga maisha ya Kanisa la mwanzo na kumuongoa mfalme huyo pamoja na wananchi wengi sana, akianzisha kwa ajili yao majimbo mbalimbali[1].

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu "mtume wa Uingereza".

Sikukuu yake ni tarehe 26 Mei au 27 Mei[2].

Tazama pia

Vyanzo vya kale

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.