From Wikipedia, the free encyclopedia
Rasi ya Antatiki ndio rasi kubwa kabisa huko Antaktiki. Ni sehemu ya kaskazini kabisa ya bara hilo.
Rasi ina urefu wa km 1300 kuanzia Rasi Adams kwenye Bahari ya Weddell hadi mwisho wake upande wa kaskazini uliopo kama km 1,000 kutoka Tierra del Fuego, sehemu ya kusini kabisa ya Amerika Kusini.
Kuna vituo vingi vya utafiti wa kisayansi kutoka mataifa mbalimbali pamoja na madai ya nchi hizi juu ya maeneo ya rasi.
Rasi yote inafunikwa na tabaka nene la barafu ya kudumu; hata hivyo ni sehemu ya Antaktiki ambako baridi ni nafuu kidogo. Wastani wa joto katika rasi hucheza kati ya sentigredi +1 hadi +2 kwenye mwezi wa Januari na °C −15 hadi −20 kwenye Juni. [1]
Kuna milima mingi inayofikia kimo cha mita 2,800. Kijiografia milima hiyo huhesabiwa kama sehemu ya kusini kabisa ya safu za Andes za Amerika Kusini.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.