From Wikipedia, the free encyclopedia
Akatistos (kwa Kigiriki: Ἀκάθιστος Ὕμνος, "utenzi usiotaka ukae"[1]) ni utenzi wa Ukristo wa mashariki kwa nafsi mojawapo ya Utatu Mtakatifu, kwa tukio fulani la kalenda ya liturujia, au kwa mtakatifu yeyote.
Akatistos maarufu zaidi ni ile iliyoandikwa katika karne ya 7 kwa heshima ya Mama wa Mungu. Mtunzi wake hajulikani kwa hakika.
Kwa sasa imeenea hata katika Kanisa la magharibi na kuna tafsiri mbili katika lugha ya Kiswahili: moja ya Waorthodoksi wa Kenya, nyingine ya Wakatoliki wa Tanzania.
Pia, kuna picha takatifu za Theotokos zinazojulikana kwa jina "Akatistos".
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.