Einigkeit und Recht und Freiheit
From Wikipedia, the free encyclopedia
Einigkeit und Recht und Freiheit ("Umoja na haki na uhuru") ni maneno ya kwanza ya wimbo wa taifa la Ujerumani. Wimbo huo ulitungwa kiasili na mshairi Hoffmann von Fallersleben mwaka 1841 kama "wimbo la Wajerumani" (Lied der Deutschen) likiwa na mabeti matatu. Lakini beti ya tatu pekee inayokubaliwa kama wimbo la taifa. Muziki yake iliandikwa na Joseph Haydn.
Beti asilia ya kwanza inajulikana kutokana na chanzo chake "Ujerumani juu ya yote" (Deutschland, Deutschland über alles) lakini baada ya maarifa ya utaifa mkali katika karne ya 20 uliopeleka nchi katika vita kuu mbili Wajerumani wengi hawapendi tena beti hii hivyo haitumiki tena.