Virusi vya kompyuta
From Wikipedia, the free encyclopedia
Virusi vya kompyuta (kwa Kiingereza: computer virus) ni programu haramu yenye uwezo wa kujisambaza ndani ya kompyuta na kujiingiza ndani ya programu halali zinazotakiwa kufanya kazi mle. Ikisambaa inaathiri programu halali na kusababisha hasara. Virusi vinasambaa kwa njia ya intaneti lakini pia kwa njia ya sidii au diski yoyote ya kubebea data kati ya kompyuta tofauti. Virusi vinaweza kuharibu mafaili na kupunguza uwezo na kasi wa ufanyaji kazi wa kompyuta.
Makala hii, au sehemu za makala hii, inahitaji vyanzo au marejeo yoyote. Tafadhali saidia kuboresha makala hii kwa kuweka vyanzo vya kuaminika. Habari zisizowekewa vyanzo zinaweza kuwekewa alama na kuondolewa. (June 2019) |