![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/d9/Ubangi_21.43546E_4.35078N.jpg/640px-Ubangi_21.43546E_4.35078N.jpg&w=640&q=50)
Ubangi
Mto wa Afrika ya Kati na tawimto la Mto Kongo / From Wikipedia, the free encyclopedia
Ubangi ni tawimto mkubwa wa mto Kongo na kati ya mito mirefu ya Afrika.
Ukweli wa haraka Mto wa Ubangi ...
Chanzo | Maungano ya mito Mbomou na Uele mpakani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |
Mdomo | Mto Kongo (karibu na Mbandaka) |
Nchi | Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo |
Urefu | 850 km, pamoja na Uele 2.272 km |
Tawimito | Mbomou, Uele |
Mkondo | 7,000 m³/s |
Eneo la beseni | 613,202 km² |
Miji mikubwa kando lake | Bangui |
Funga
Chanzo chake ni maungano ya mito Mbomou na Uele kwenye mpaka wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (J.A.K.) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (J.K.K.).
Mto waelekea kwanza magharibi halafu magharibi-kusini ukipitia mji mkuu Bangui.
Mwendo wote wa mto Ubangi ni mpaka wa kimataifa: kwanza kati ya J.A.K. na J.K.K., halafu kati ya J.K.K. na Jamhuri ya Kongo.
Ubangi waishia katika mto Kongo takriban kilomita 90 kusini kwa mji wa Mbandaka.