Tuul (mto)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tuul (kwa Kimongolia: Туул гол) ni mto muhimu wa Mongolia. Mto una urefu wa km 704 na beseni la km² 49,840.
Chanzo chake ni ambapo matawimto ya Namiya na Nergui inaungana kwenye mtelemko wa mlima Khentei. Tuul inapeleka maji yake kwenda ziwa Baikal kupitia mto Selenge. Inapita katika mji mkuu Ulanbaatar.
Beseni la Tuul ni asilimia 3.19 tu za eneo la Mongolia lakini zaidi ya nusu ya wakazi wa nchi huishi humo.