![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/c/c9/Sphere_wireframe_10deg_3r.svg/langsw-640px-Sphere_wireframe_10deg_3r.svg.png&w=640&q=50)
Tufe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tufe ni umbo la gimba linalofanana na mpira au chungwa. Lakini wala mpira wala chungwa ni tufe kamili.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/c/c9/Sphere_wireframe_10deg_3r.svg/640px-Sphere_wireframe_10deg_3r.svg.png)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/07/Sphere_and_Ball.png/640px-Sphere_and_Ball.png)
Katika elimu ya hisabati, hasa jiometri tufe ni jumla la nukta zote zilizopo na umbali uleule (=rediasi, nusukipenyo) kutoka nukta nukta moja (kitovu cha tufe).
Tufe ni mzunguko wa duara katika wanda (dimension) la tatu.
- Kitovu cha tufe ni nukta iliyopo katikati yake yenye umbali sawa na kila nukta kwenye uso wake.
- Nusukipenyo cha tufe ni umbali kati ya kitovu chake hadi nukta yoyote kwenye uso wake
- Uso wa tufe ni eneo linalojumlisha nukta zote zenye umbali wa nusukipenyo kutoka kitovu