From Wikipedia, the free encyclopedia
Tufani (kutoka neno la Kiarabu) ni dhoruba yenye mwendo wa kuzunguka. Inasababishwa na eneo la shindikizo duni la hewa ambako upepo umeanza kuzunguka ndani yake.
Mzunguko huu hufuata mwendo wa saa katika maeneo ya kusini kwa ikweta na huenda kinyume cha mwendo wa saa katika maeneo ya kaskazini kwa ikweta.
Tufani ikitokea kwenye nchi kavu huitwa chamchela.
Kwenye bahari za tropiki mzunguko unaongezeka nguvu kutoka nishati ya joto ya maji baharini kuwa dhoruba kali. Tufani hizi zinazoanza baharini huitwa kimbunga. Kimataifa kuna majina mengine yaliyo tofauti kila bahari kama vile:
Tufani zimetazamwa pia katika falaki kwenye sayari za mfumo wa jua letu kama Mshtarii na Meriki. Hasa doa jekundu kubwa lililoonekana kwenye Mshtarii tangu mwaka 1830 na hata kabla ya hapo limetambuliwa kuwa tufani.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tufani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.