Tarumbeta
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tarumbeta ni ala ya muziki ya kupuliza ikitengenezwa kwa metali hasa shaba nyeupe. Upande wa mdomo ni nyembamba na upande wa mwisho ni pana yenye. Urefu wa bomba lake linaweza kukaribia mita 1 na nusu lakini bomba hili limepindwa mara mbili kwa kuwa na ala isiyo ndefu mno. Katikati huwa na vilango 3 vinavyobadilisha njia ya hewa na kusababisha sauti kuwa juu na chini.
Sauti yenyewe haufanywi na tarumpeta -tofauti na filimbi- lakini kwa kupuliza hewa baina ya midomo iliyokazwa ndani ya mdomo wa tarumpeta. Ala inapazia sauti hii na kuibadilisha.