Tanbihi (kwa Kiingerezafootnotes au endnotes) ni maelezo ya nyongeza kuhusu matini yanayoandikwa ama chini ya kila ukurasa, mwishoni mwa mlango au pia mwishoni kabisa mwa makala au kitabu.
Matini ya makala ya swwiki Akarabu (kundinyota) inayoonyesha namba za tanbihi yaani maelezo mwishoni mwa makala yanakayothibitisha maelezo katika matini
Tanbihi chini ya makala ya enwiki en:Tippu Tipp zinaonyesha maelezo kuhusu matamko katika matini mfululizo wa makala. Tanbihi ziko za aina mbalimbali, ama kama kiunganishi (link) kwa tovuti nyingine nje ya wikipedia au kwa kutaja makala au kitabu pamoja na habari zake (mwandishi, tarehe, makala katika jarida gani, na kadhalika)
Maelezo ya tanbihi huandikwa nje ya matini inayoendelea ili kurahisisha kazi ya kusoma.