Buabua ni ndege wa familia Sternidae. Watu wengi huita ndege hawa shakwe kama spishi za familia Laridae. Wengine hutumia jina buabua kwa spishi za jenasi Anous na Chlidonias. Spishi za jenasi Gygis ni nyeupe kabisa, zile za Sterna ni nyeupe na zina utosi weusi; spishi nyingi zina madoa meusi kwa mabawa pia. Spishi za Chlidonias zina zaidi ya rangi nyeusi, hata kwa mwili wao, na spishi za Anous zina rangi nyeupe chache tu. Buabua wana domo refu kadiri lenye ncha kali. Wanaweza kuogelea na wana ngozi kati ya vidole vyao.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Buabua |
Buabua domo-kubwa |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Ngeli: |
Aves (Ndege)
|
Oda: |
Charadriiformes (Ndege kama vitwitwi)
|
Familia: |
Sternidae (Ndege walio na mnasaba na buabua)
|
Jenasi: |
Anous Stephens, 1826
Chlidonias Rafinesque, 1822
Gelochelidon Brehm, 1830
Gygis Wagler, 1832
Hydroprogne Kaup, 1829
Larosterna Blyth, 1852
Onychoprion Wagler, 1832
Phaetusa Wagler, 1832
Procelsterna Lafresnaye, 1842
Sterna Linnaeus, 1758
Sternula Gould, 1843
Thalasseus Boie, 1822
|
|
Funga
Kama shakwe, buabua huhusiswha na pwani, lakini spishi nyingi wanatokea mbali na bahari, kwa kawaida karibu na maji. Huwakamata samaki wakipiga mbizi, lakini spishi za Chlidonias huwakamata wadudu pia kutoka juu ya maji baridi. Hulitengeneza tago lao chini, mara nyingi kisiwani.
- Anous minutus, Buabua Mweusi (Black Noddy)
- Anous stolidus, Buabua Kahawia (Brown Noddy)
- Anous tenuirostris, Buabua Domo-jembamba (Lesser Noddy)
- Chlidonias hybridus, Buabua Masharubu (Whiskered Tern)
- Chlidonias leucopterus, Buabua Mabawa-meupe (White-winged Tern)
- Chlidonias niger, Buabua Mabawa-kijivu (Black Tern)
- Gelochelidon nilotica, Buabua Domo-nene (Gull-billed Tern)
- Gygis alba, Buabua Mweupe (White Tern au White Noddy)
- Hydroprogne caspia, Buabua Domo-kubwa (Caspian Tern)
- Onychoprion anaethetus, Buabua Mgongo-kijivu (Bridled Tern)
- Onychoprion fuscatus, Buabua Mgongo-mweusi (Sooty Tern)
- Sterna dougallii, Buabua Mkia-mshale (Roseate Tern)
- Sterna hirundo, Buabua Mbayuwayu (Common Tern)
- Sterna paradisaea, Buabua wa Akitiki (Arctic Tern)
- Sterna repressa, Buabua Mashavu-meupe (White-cheeked Tern)
- Sterna sumatrana, Buabua Kisogo-cheusi (Black-naped Tern)
- Sterna virgata, Buabua wa Kerguelen (Kerguelen Tern)
- Sterna vittata, Buabua wa Antakitiki (Antarctic Tern)
- Sternula albifrons, Buabua Kibete (Little Tern)
- Sternula balaenarum, Buabua wa Damara (Damara Tern)
- Sternula saundersi, Buabua wa Saunders (Saunders’s Tern)
- Thalasseus bengalensis, Buabua Kishungi Mdogo (Lesser Crested Tern)
- Thalasseus bergii, Buabua Kishungi Mkubwa (Greater Crested Tern)
- Thalasseus maximus, Buabua Mfalme (Royal Tern)
- Thalasseus sandvicensis, Buabua Domo-rangimbili (Sandwich Tern)
Buabua mweusi
Buabua kahawia
Buabua domo-jembamba
Buabua masharubu
Buabua mabawa-meupe
Buabua mabawa-kijivu
Buabua domo-nene
Buabua mweupe
Buabua domo-kubwa
Buabua mgongo-kijivu
Buabua mgongo-mweusi
Buabua mkia-mshale
Buabua mbayuwayu
Buabua wa Akitiki
Buabua mashavu-meupe
Buabua kisogo-cheusi
Buabua wa Kerguelen
Buabua wa Antakitiki
Buabua kibete
Buabua kishungi mdogo
Buabua kishungi mkubwa
Buabua mfalme
Buabua domo-rangimbili
Inca tern
Grey-backed tern
Grey noddy
Blue noddy
River tern
Forster’s tern
White-fronted tern
Least tern
Yellow-billed tern
Elegant tern