Spaghetti
From Wikipedia, the free encyclopedia
Spageti (kwa Kiitalia: Spaghetti) ni chakula cha tambi chenye asili ya Italia Kusini. Ni tambi ya ngano yenye umbo jembamba kama kamba na urefu wa sentimeta 40.
Hupikwa katika maji kwa dakika chache na kuliwa kwa uma baada ya kuongeza michuzi mbalimbali.
Spageti ni aina mojawapo ya chakula cha pasta na neno latumiwa wakati mwingine kutaja pasta kwa jumla.
Kutoka Italia chakula hiki kimeenea duniani kote kwa sababu hupikwa haraka, inaleta shibe nzuri na kuna njia nyingi za kubadilisha ladha yake.
Kwa njia ya utani zimekuwa ishara ya utamaduni wa Italia, jinsi inavyoonekana katika filamu za Spaghetti Western.