Usubi weusi (pia visubi weusi au nzi weusi) ni mbu wadogo wa familia Simuliidae katika oda Diptera wanaofyonza damu. Spishi fulani hueneza upofu wa mtoni unaoitwa usubi pia. Kuna visubi wengine walio wana wa familia Ceratopogonidae na wa nusufamilia Phlebotominae katika familia Psychodidae. Visubi hao hufyonza damu pia na kueneza magonjwa.
Usubi mweusi | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Usubi mweusi (Simulium sp.) | ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Nusufamilia 2:
| ||||||||||||||||||
Mbu hawa ni wadogo, mm 5-15. Kwa kawaida rangi yao ni nyeusi au kijivu. Vipapasio ni vifupi. Toraksi (kidari) imepindika na kwa hivyo kichwa kinaelekea chini.
Madume ya usubi weusi hula mbochi lakini majike yanahitaji damu, iliyo na kiwango juu cha protini, ili mayai yaendelee. Spishi nyingi sana hufyonza damu ya mamalia lakini spishi nyingine hufyonza damu ya ndege.
Spishi nyingi za usubi weusi hueneza vidusia vya mamalia na ndege. Katika Afrika wanapishia watu vinyoo wa Onchocerca volvulus tu lakini katika Amerika ya Kusini na ya Kati wanaeneza vinyoo wa Mansonella ozzardi pia. Dalili za wale wa mwisho si mahututi sana kwa kawaida. Kwa upande mwingine O. volvulus anasababisha upofu wa mtoni. Katika Afrika ya Mashariki hupishwa na Simulium damnosum na S. neavei.
Jina la upofu wa mtoni linatokana na mtazamo kama watu wanaoteseka na ugonjwa huu huishi karibu na mito. Sababu yake ni kwamba lava wa usubi weusi huishi majini kwa mito yenye mtiririko mkali. Kitembo cha kuokoka ni nyeti sana kwa kiwango cha uchafuzi wa maji. Mabuu hutumia ndoana ndogo kwenye ncha ya tumbo lao kushikilia dutu ya chini wakitumia mishikilizo na nyuzi za hariri kusogea au kushikilia mahali pao. Wana vipepeo vidogo vinavyoweza kukunjwa kuzunguka kinywa chao. Vipepeo hujitanua wakati wa kujilisha na kukamata vifusi vinavyopita (chembe ndogo za viumbehai, viani na bakteria). Mabuu hukwangua vitu vilivyokamatwa kutoka vipepeo ndani ya kinywa chao kila sekunde chache. Usubi weusi hutegemea makao ya mito yanayowaletea chakula. Hugeuka kuwa mabundo chini ya maji na kisha hutoka ndani ya kiputo cha hewa kama wapevu wanaoruka. Mara nyingi hutekwa na trouti au samaki wengine wakati wa kuibuka.
Spishi kadhaa za Afrika ya Mashriki
- Simulium damnosum
- Simulium kenyae
- Simulium mcmahoni
- Simulium neavei
Picha
- Usubi mweusi akifyonza damu
- Mchoro wa lava
- Lava na mabundo
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.