From Wikipedia, the free encyclopedia
San Marino (kwa Kiitalia maana yake ni "Mtakatifu Marino") ni kati ya nchi ndogo kabisa duniani. Eneo lake lote limo ndani ya mipaka ya Italia, kati ya wilaya za Rimini na Pesaro-Urbino, karibu na mwambao wa bahari ya Adria.
San Marino |
---|
San Marino inatajwa kuwa jamhuri yenye umri mkubwa kuliko zote duniani. Ilianzishwa na Wakristo waliokimbia dhuluma ya Kaisari wa Roma Diokletiano wakitafuta kimbilio mlimani.
Kati yao, shemasi Marino na padri Leo ndio maarufu zaidi.
Tangu hapo imefaulu kudumisha uhuru wake. Ndiyo sababu tangu mwaka 2008 imeorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia.
San Marino ina wakazi 33,909 (2019) katika vijiji 9. Karibu wote (97.2%) ni waumini wa Kanisa Katoliki (jimbo la San Marino-Montefeltro) na wanaongea Kiitalia kwa lahaja ya Kiromagna.
San Marino imetunza utaratibu wa serikali inayofanana na muundo wa jamhuri ya Roma ya kale. Serikali inaongozwa na watawala wawili ("Capitani Reggenti") wanaochaguliwa kwa muda wa miezi sita tu kama zamani konsuli wa Kiroma.
Bunge linaitwa Halmashauri Kuu ("Consiglio Grande e Generale") likichaguliwa kila baada ya miaka mitano. Halmashauri inateua pia kamati ya watu 12 ("Consiglio dei XII") inayotekeleza kazi ya mahakama.
Wananchi wote hukutana mara mbili kwa mwaka kama mkutano mkubwa wa "Arengo" wakiamua juu ya matamko na mapendekezo kwa serikali.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu San Marino kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.