Sahara ya Magharibi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sahara ya Magharibi ni eneo la Afrika ya Kaskazini-Magharibi kwenye mwambao wa Bahari Atlantiki upande wa magharibi.
| |||||
Lugha rasmi | Kiarabu na Kihispania | ||||
Mji mkuu | El Aaiún | ||||
Mji mkubwa | El Aaiún | ||||
Rais (wa nje) |
Mohamed Abdelaziz | ||||
Waziri Mkuu (wa nje) | Abdelkader Taleb Oumar | ||||
Eneo - Jumla - % maji |
266 000 km² -- | ||||
Wakazi - Jumla - Msongamano wa watu |
548,000 (Julai 2003) 1/km² | ||||
Uhuru - ilitangazwa - Nchi kutwaliwa |
na Hispania 27 Februari 1976 na Moroko | ||||
Pesa | Dirham ya Moroko | ||||
Wakati | UTC 0 | ||||
Wimbo la taifa | ? | ||||
TLD (mtandaoni) | -- (.eh iliwekwa tayari) | ||||
simu ya kimataifa | + 212. (kama Moroko) |
Imepakana na Moroko upande wa kaskazini, Algeria upande wa mashariki na Mauretania upande wa kusini.
Ilitangazwa nchi huru mwaka 1976 kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Sahara lakini kwa kiasi kikubwa inatawaliwa na Moroko kama mikoa yake ya kusini.
Nchi nyingi za dunia pamoja na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika hazitambui Sahara Magharibi kuwa sehemu ya Moroko. Nchi 53 zinaikubali kama Jamhuri huru. Hali halisi sehemu kubwa ya ardhi yake inatawaliwa na Moroko inayodai ni sehemu ya eneo lake la kitaifa.
Sehemu kubwa ya wakazi asilia wako nje ya eneo kama wakimbizi katika makambi makubwa nchini Algeria.