![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/23/Noahs_Ark.jpg/640px-Noahs_Ark.jpg&w=640&q=50)
Safina
From Wikipedia, the free encyclopedia
Safina ya Noah (kutoka Kiarabu: سفينة نوح, Safina Nuh; kwa Kiebrania ni: תיבת נח, Tevat Noaḥ) ni chombo kikubwa ambamo, kadiri ya simulizi la Kitabu cha Mwanzo (Biblia), Noah na familia yake walikombolewa wakati wa gharika kuu.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/23/Noahs_Ark.jpg/640px-Noahs_Ark.jpg)
Pamoja nao wanyama wa kila aina waliokolewa humo wasife maji.
Kadiri ya kitabu hicho cha Agano la Kale, sura 6-9, Mungu ndiye aliyemuagiza Noah atengeneze chombo hicho.
Habari hiyo inapatikana pia, kwa tofauti kadhaa, katika Quran.