![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/8/82/Jos%25C3%25A9_de_Ribera_012.jpg/640px-Jos%25C3%25A9_de_Ribera_012.jpg&w=640&q=50)
Rebeka
From Wikipedia, the free encyclopedia
Rebeka (kwa Kiebrania רבקה, Rivqah) alikuwa binamu na mke wa Isaka ambaye, baada ya utasa wa muda mrefu, hatimaye alimzalia watoto pacha Esau (au Edomu, babu wa Waedomu) na Yakobo Israeli (babu wa Waisraeli).
![Spagnoletto: Yakobo akiibia baraka ya Isaka kwa msaada wa Rebeka (1637), Prado, Madrid (Hispania).](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/8/82/Jos%C3%A9_de_Ribera_012.jpg/640px-Jos%C3%A9_de_Ribera_012.jpg)
Kwa ujanja wake alifaulu kumfanya mume wake atoe baraka iliyokuwa haki ya mtoto wa kwanza kwa mdogo wake.
Anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Septemba.