From Wikipedia, the free encyclopedia
Pato la taifa au jumla ya pato la taifa (kifupi: JPT) ni kipimo cha thamani ya sokoni ya bidhaa na huduma zote zinazozalishwa ndani ya nchi katika muda fulani.[1]
JPT hutumiwa kwa kawaida na serikali ya nchi ili kupima afya ya uchumi wake. Kipimo hicho mara nyingi hurekebishwa kabla ya kufikiriwa kuwa kiashiria cha kuaminika.[2]
Pato kamili, yaani pato lisilorekebishwa, halihesabu gharama za maisha zinazotofautiana nchi kwa nchi. Kwa hiyo, wachumi mara nyingi hutoa taarifa ya pato halisi la taifa. Thamani hiyo ndiyo inayohesabu tofauti za uwezo wa ununuzi unaosababishwa na gharama za maisha. Pato halisi la taifa hupatwa kwa kukokotoa kima cha uwezo sawa wa ununuzi.[3]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.