Pathojeni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Pathojeni (au kiambukizi; kwa Kiingereza: pathogen, kutoka Kigiriki: πάθος pathos “mateso” na -γενής -genēs “kuzaa”) ni kile kinachosababisha ugonjwa. Kwa kawaida ni vidubini kama vile bakteria, virusi, fungi au vimelea vinavyoweza kusababisha maradhi. Vidubini hivyo vyote ni vidogo mno, havionekani na macho.
Hata hivyo, si kila bakteria au fungi anasababisha ugonjwa, kinyume chake tunaishi kwa kuwa na mamilioni ya bakteria katika utumbo ambao ni lazima kuwepo kwa afya yetu.