Domofupi ni ndege wa familia Paridae. Hawa ni ndege wadogo wenye domo fupi na mkia mfupi; spishi kadhaa zina kishungi. Rangi zao si kali sana: kwa kawaida nyeusi, nyeupe, kijivu na/au kahawia, pengine buluu, njano na nyekundu. Wanatokea Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Kaskazini katika maeneo yenye miti. Hula wadudu na pia mbegu na makokwa. Hulijenga tago lao ndani ya tundu mtini. Jike huyataga mayai 3-19 yenye madoa.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Domofupi |
Domofupi tumbo-jeupe |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Nusufaila: |
Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
|
Ngeli: |
Aves (Ndege)
|
Oda: |
Passeriformes (Ndege kama shomoro)
|
Familia ya juu: |
Sylvioidea (Ndege kama kucha)
|
Familia: |
Paridae (Ndege walio na mnasaba na domofupi)
|
|
Ngazi za chini |
Jenasi 14:
- Baeolophus Cabanis, 1850
- Cephalopyrus Bonaparte, 1854
- Cyanistes Kaup, 1829
- Lophophanes Kaup, 1829
- Machlolophus Cabanis, 1850
- Melaniparus Bonaparte, 1850
- Melanochlora Lesson, 1839
- Pardaliparus De Sélys Longchamps, 1884
- Parus Linnaeus, 1758
- Periparus De Sélys Longchamps, 1884
- Poecile Kaup, 1829
- Pseudopodoces Zarudny & Loudon, 1902
- Sittiparus De Sélys Longchamps, 1884
- Sylviparus Burton, 1836
|
Funga
- Cyanistes teneriffae, Domofupi Buluu wa Afrika (African blue tit)
- Melaniparus afer, Domofupi Kusi (Grey tit)
- Melaniparus albiventris, Domofupi Tumbo-jeupe (White-bellied tit)
- Melaniparus carpi, Domofupi wa Carp (Carp's tit)
- Melaniparus cinerascens, Domofupi Kijivu (Ashy tit)
- Melaniparus fasciiventer, Domofupi Tumbo-baka (Stripe-breasted Tit)
- Melaniparus fringillinus, Domofupi Koo-jekundu (Red-throated tit)
- Melaniparus funereus, Domofupi Macho-mekundu (Dusky tit)
- Melaniparus griseiventris, Domofupi-miyombo (Miombo tit)
- Melaniparus guineensis, Domofupi Mabega-meupe (White-shouldered black tit]
- Melaniparus leucomelas, Domofupi Mabawa-meupe (White-winged black tit)
- Melaniparus leuconotus, Domofupi Mgongo-mweupe (White-backed black tit)
- Melaniparus niger, Domofupi Mweusi Kusi (Southern black tit)
- Melaniparus pallidiventris, Domofupi Kidari-marungi (Cinnamon-breasted tit)
- Melaniparus rufiventris, Domofupi Tumbo-jekundu (Rufous-bellied tit)
- Melaniparus thruppi, Domofupi Somali (Acacia au Somali tit)
- Parus major, Domofupi Mkubwa (Great tit)
- Periparus ater, Domofupi Mweusi Kaskazi (Coal tit) – labda spishi kadhaa
- Periparus a. atlas, Domofupi wa Atlasi (Coal tit)
- Periparus a. ledouci, Domofupi wa Aljeria (Coal tit)
Domofupi buluu wa Afrika
Domofupi kusi
Domofupi wa Carp
Domofupi kijivu
Domofupi tumbo-baka
Domofupi-miyombo
Domofupi mabawa-meupe
Domofupi mweusi kusi
Domofupi tumbo-marungi
Domofupi tumbo-jekundu
Domofupi mkubwa
Domofupi mweusi kaskazi