From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Silvester I alikuwa Papa kuanzia tarehe 31 Januari 314 hadi kifo chake tarehe 31 Desemba 335[1].
Alimfuata Papa Miltiades akafuatwa na Papa Marko.
Mtoto wa Rufinus, mkazi wa Roma, hatuna habari nyingi za maisha yake. Ila ni kwamba aliongoza Kanisa Katoliki kwa muda mrefu mara baada ya Kaisari Konstantino Mkuu kulipatia uhuru wa dini na kulijengea maabadi mengi, makubwa na mazuri.
Wakati wa utawala wake ulifanyika mtaguso mkuu wa kwanza (Nisea, leo nchini Uturuki, 325). Yeye hakuhudhuria, ila alituma wajumbe wawili akathibitisha maamuzi yaliyofikiwa.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.