From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Gregori III alikuwa Papa kuanzia tarehe 18 Machi 731 hadi kifo chake tarehe 28 Novemba 741[1].
Alizaliwa katika nchi ya Syria[2], akiwa Papa wa mwisho kutokea nje ya Ulaya hadi alipochaguliwa Papa Fransisko mwaka 2013[3]. Baba yake aliitwa Yohane[4].
Alimfuata Papa Gregori II akafuatwa na Papa Zakaria.
Mara baada ya kuchaguliwa na umati wa waumini [5] na kuthibitishwa na mwakilishi wa kaisari wa Dola la Roma Mashariki[6] alimsihi Kaisari Leo III alegeze msimamo wake wa kupinga matumizi ya picha takatifu. Kwa kuwa balozi wake alikamatwa, Papa aliitisha Sinodi ya Roma (731) iliyolaani vikali msimamo huo[7].
Pamoja na maamuzi mengine, Papa Gregori III alimfanya mmisionari Bonifas kuwa askofu mkuu na balozi wake huko Ujerumani[8]. Vilevile aliunga mkono kazi ya Wilibaldi hukohuko [9]
Alipaswa pia kupambana na uvamizi wa Walombardi katika Italia ya Kati akitegemea kwanza msaada wa kaisari, halafu ule wa Wafaranki, ambao hata hivyo hawakuitikia sana.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 10 Desemba[10].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.