From Wikipedia, the free encyclopedia
Ole Christensen Rømer (matamshi ya Kidenmark: [ˈOːlə ˈʁœˀmɐ] ; 25 Septemba 1644 - 19 Septemba 1710) alikuwa mtaalamu wa astronomia kutoka Denmark ambaye mnamo 1676 alifanya vipimo vya kwanza vya Kasi ya nuru.
'
Ole Rømer | |
---|---|
Ole Rømer | |
Amezaliwa | 25 Septemba 1644 |
Amefariki | 19 Septemba 1710 |
Kazi yake | mtaalamu wa astronomia kutoka Denmark |
Rømer pia alibuni kipimajoto cha kisasa kinachoonyesha halijoto kati ya nukta mbili ambazo ni sehemu ambapo maji huchemka na kuganda.
Katika vitabu vya sayansi, tahajia mbadala kama "Roemer", "Römer", au "Romer" ni kawaida.
Rømer alizaliwa mnamo 25 Septemba 1644 mjini Aarhus. Wazazi wake walikuwa mfanyabiashara na nahodha Christen Pedersen (aliyefariki 1663), na Anna Olufsdatter Storm (1610 hivi - 1690), binti wa mjumbe wa halmashauri ya mji. [1] Tangu mwaka 1642, Christen Pedersen alikuwa akitumia jina la Rømer, ambalo linamaanisha kwamba alitokea kisiwa cha Denmark cha Rømø, ili kujitofautisha na watu wengine kadhaa walioitwa pia Christen Pedersen. [2]
Kuna habari chache kuhusu Ole Rømer kabla ya 1662, alipohitimu kutoka kwa shule ya kanisa kuu la Aarhus.[3] Kutoka hapo alihamia Kopenhagen akasoma hisabati na astronomia kwenye Chuo Kikuu cha Kopenhagen . Mlezi wake kwenye Chuo Kikuu alikuwa profesa Rasmus Bartholin alieyechapisha ugunduzi wake wa upindaji maradufu ya mwanga katika fuwele mnamo 1668, wakati Rømer alikuwa akiishi nyumbani kwake. Rømer alipewa fursa ya kujifunza hisabati na astronomia akitumia maandiko ya Tycho Brahe, kwani Bartholin alikuwa amepewa jukumu la kuyaandaa kwa uchapishaji. [4]
Baada ya kuhitimu chuo Rømer aliajiriwa na serikali ya Ufaransa: mfalme Louis XIV alimfanya mwalimu wa mwanawe alishiriki pia katika ujenzi wa chemchemi za mapambo nzuri kwenye jumba la Versailles .
Mnamo 1681 Rømer alirudi Denmark akateuliwa kuwa profesa wa astronomia katika Chuo Kikuu cha Kopenhagen.
Rømer alipewa pia nafasi ya mwanahisabati mkuu wa kifalme na hapo alianzisha mfumo wa kwanza wa kitaifa wa vipimo sanifu katika Denmark mnamo 1 Mei 1683. [5] [6] Pamoja na vipimo vingine alifafanua mailimpya ya Kidenmark kuwa na futi 24,000 (karibu mita 7,532 ). [7]
Mnamo mwaka 1700 Rømer alimshawishi mfalme kukubali kalenda ya Gregori kwa matumizi katika ufalme wa Denmark-Norwei. Hili ni jambo ambalo Tycho Brahe alishindwa kuanzisha miaka mia moja kabla yake. [8]
Rømer alibuni moja ya skeli za kupima halijoto za kwanza.[9] Daniel Gabriel Fahrenheit alimtembelea mnamo 1708 na kuendeleza skeli ya Rømer, na matokeo yake yalikuwa skeli ya joto ya Fahrenheit inayotumika hadi leo katika nchi kadhaa ingawa mahali pengi skeli ya selsiasi imechukua kipaumbele. [10] [11] [12]
Rømer pia alianzisha vyuo kwa mabaharia katika miji kadhaa ya Denmark. [13]
Mnamo mwaka wa 1705, Rømer alipewa pia kazi ya kusimamia polisi ya Kopenhagen, nafasi ambayo aliishikilia hadi kifo chake mnamo 1710. [14] Kama moja ya maazimio yake ya kwanza, alifukuza watumishi wote wote, akiamini kuwa ari yao ilikuwa duni mno. Alibuni taa za kwanza za barabarani (taa za mafuta) mjini Kopenhagen. Alijitahidi kudhibiti waombaomba, watu wasio na kazi, na makahaba wa Kopenhagen. [15] [16]
Rømer alitunga sheria za ujenzi wa nyumba mpya, akatengeneza mfumo wa maji na maji taka ya mji, akapatia walinzi moto vifaa vipya akashawishi serikali ya mji kupanga mitaa imara iliyofunikwa kwa mawe ya vibbamba. [17] [18] [19]
Rømer alifaRIKI akiwa na umri wa miaka 65 mnamo 1710. Alizikwa katika Kanisa Kuu la Kopenhagen.[20]
Hadi siku za Romer wataalamu wengi waliona nuru haina kasi, wakiamini inafika mara moja kwa mtazamaji. Lakini wengine walihisi inaweza kuwa na mwendo.
Mnamo 1671 Rømer akajiunga na Jean Picard kutazama kupatwa kwa Io, mwezi wa Mshtarii, kwa kipindi cha miezi kadhaa, wakati Giovanni Domenico Cassini alitazama matukio ya kupatwa yaleyale huko Paris, Ufaransa. Io inazunguka Mshtarii kila baada masaa 42½ kwa hiyo kwa mtazamaji wa duniani inafunikwa na sayari hiyo kwa sehemu ya obiti yake, yaani inapatwa na Mshtarii.
1668 Cassini aliwahi kutoa jedwali inayotabiri ufuatano na wakati wa kuona kupatwa kwa Io. Lakini wakati wa kutazama Io na Mshtarii kuna tofauti ya dakika kadhaa kati ya jedwali yake na kupatwa jinsi kunavyotazamwa.
Rømer alitambua kwamba mabadiliko haya yako tofauti kulingana na majira ya mwaka. Romer aliamini kwamba kasi ya obiti ya Io haibadiliki; ilhali alijua umbali kati ya Mshtarii na Dunia inayobadilika kidogo kulingana na mwendo wao zikizunguka Jua, alitambua kwamba wakati Dunia na Mshtarii zinaongeza umbali kati yake, muda wa kupatwa ulikuwa mkubwa kidogo. Kinyuma chake wakati Dunia na Mshtarii zinasogea karibu zaidi, muda wa kupatwa wa Io ulipungua kidogo.
Rømer aliwaza kwamba vipimo hivi vinaweza kuelezwa kama nuru ina kasi maalumu aliyoendelea kukadiria. Aliona nuru ilitembea kati ya dakika 10 hadi 11 kutoka Io hadi duniani, kutegemeana na umbali.
Wakati wa maisha yake, wataalamu bado walivutana kati yao kama nuru kweli ina kasi. Lakini hasa pale Uingereza wanaastronomia kama Christiaan Huygens na Isaac Newton walivutwa na makadirio ya Romer na kwa kutumia hesabu zake waliweza tayari kupiga hesabu kuwa nuru ya Jua inahitaju takriban dakika nane kufika duniani, na kipimo hiki kilifanana tayari na elimu yetu ya leo.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.