Nzi-gome
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nzi-gome (kutoka Kiing.: barkfly) ni wadudu wadogo (mm 1-10) wa oda Psocodea (psokhos = iliyotafunwa, ptera = mabawa) katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Spishi zinazoishi ndani ya majengo huitwa chawa-vitabu. Zamani spishi fulani za nusuoda Troctomorpha ziligeuka kuwa chawa vidusia. Kwa hivyo siku hizi wataalamu wanaweka chawa katika Psocodea kama oda ndogo Phthiraptera chini ya Troctomorpha.
Nzi-gome | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Metylophorus nebulosus | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Nusuoda 3:
| ||||||||||||
Wadudu hawa wana mwili kwa muundo wa msingi. Paji ya kichwa imefura, macho ni makubwa kwa kulinganisha na wana oseli tatu. Mandibuli ni kwa kutafuna na ndewe ya kati ya maxila imegeuka katika kifito ambacho kinakaza mdudu akiparua mboji. Wakiwa na mabawa, haya huwekwa kama hema. Pengine urefu wa yale ya mbele ni 50% zaidi ya yale ya nyuyma.