Nord-Trøndelag
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nord-Trøndelag ("Trøndelag kaskazini") ni moja kati ya majimbo ya Norwei. Jimbo lipo upande wa kaskazini mwa Trøndelag. Na kwa mwaka wa 2010, jimbo lina wakazi takriban 131,555, inaifanya liwe jimbo la nne kwa uchache wa wakazi jimboni. Manispaa kubwa jimboni hapa ni pamoja na Stjørdal, Steinkjer—makao makuu wa jimbo, Levanger, Namsos na Verdal, Yote yakiiwa na idadi ya wakazi kati ya 21,000 na 12,000. Msingi wa uchumi katika jimbo hili hasa hutegemea huduma kadhaa zinazopatikana kwa viwanda, kilimo, samaki, umeme wa haidroliki na kadhalika. Jimbo lina mapato madogo sana kuliko jimbo lolote nchini humo.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/9d/Norway_Counties_Nord-Tr%C3%B8ndelag_Position.svg/640px-Norway_Counties_Nord-Tr%C3%B8ndelag_Position.svg.png)