Njiri ni ndege wadogo wa jenasi Nesocharis, Nigrita na Parmoptila katika familia Estrildidae ambao wanatokea Afrika tu. Wanafana na mishigi wenye rangi za nyeusi, kijivu na kahawia, pengine nyekundu au buluu. Hula wadudu, matunda madogo na mbegu. Tago lao ni tufe la manyasi, nyuzinyuzi na vigoga lenye mwingilio kwa kando. Jike huyataga mayai 3-6.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Njiri |
Dume la njiri utosi-kijivu |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Ngeli: |
Aves (Ndege)
|
Oda: |
Passeriformes (Ndege kama shomoro)
|
Familia ya juu: |
Passeroidea (Ndege kama shomoro)
|
Familia: |
Estrildidae (Ndege walio na mnasaba na mishigi) Bonaparte, 1850 |
|
Ngazi za chini |
Jenasi 3, spishi 10:
- Nesocharis Alexander, 1903
- N. ansorgei (Hartert. 1899)
- N. capistrata (Hartlaub, 1861)
- N. shelleyi Alexander, 1903
- Nigrita Strickland, 1843
- N. bicolor (Hartlaub, 1844)
- Nigrita canicapillus (Strickland, 1841)
- N. fusconotus Fraser, 1843
- N. luteifrons J.Verreaux & E.Verreaux, 1851
- Parmoptila Cassin, 1859
- P. jamesoni (Shelley, 1890)
- P. rubrifrons (Sharpe & Ussher, 1872)
- P. woodhousei Cassin, 1859
|
Funga
- Nesocharis ansorgei, Njiri Mkufu-mweupe (White-collared Oliveback)
- Nesocharis capistrata, Njiri mashavu-meupe (Grey-headed Oliveback)
- Nesocharis shelleyi, Njiri Kichwa-cheusi (Shelley's Oliveback)
- Nigrita bicolor, Njiri Kidari-kahawiachekundu (Chestnut-breasted Negrofinch)
- Nigrita canicapillus, Njiri Utosi-kijivu (Grey-headed Negrofinch)
- Nigrita fusconotus, Njiri Kidari-cheupe (White-breasted Negrofinch)
- Nigrita luteifrons, Njiri Paji-njano (Pale-fronted Negrofinch)
- Parmoptila jamesoni, Njiri wa Jameson (Jameson's Antpecker)
- Parmoptila rubrifrons, Njiri Paji-jekundu (Red-fronted Antpecker)
- Parmoptila woodhousei, Njiri Koo-jekundu (Woodhouse's Antpecker)