Ngome ya Yesu
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ngome ya Yesu (pia: Boma la Yesu; kwa Kiingereza: Fort Jesus) ni ngome ya kale mjini Mombasa (Kenya). Iko kwenye kisiwa cha Mombasa ikitazama mlango wa bandari ya kale.
Ilijengwa mwaka 1593 na msanifu Giovanni Battista Cairato kwa niaba ya Wareno na ilikuwa kituo muhimu cha Wareno kwenye njia ya mawasiliano kati ya Ureno na Uhindi. Jahazi zao zilipita Afrika Kusini zikapumzika kidogo Msumbiji penye ngome kubwa ya Kireno halafu ziliendelea kupitia Mombasa na kuvuka bahari hadi Bara Hindi.
Mabwana wa ngome walibadilishana.
Baada ya kuondolewa na Waomani Wareno walisafiri moja kwa moja kati ya Msumbiji na Goa.
Baada ya Wareno utawala wa ngome ulipiganiwa kati ya Sultani wa Omani na maliwali wa Mombasa wa nasaba ya Mazrui waliojaribu kuendelea bila mabwana wa Omani.
1856 Mombasa pamoja na Boma la Yesu ilikuwa sehemu ya usultani wa Zanzibar
1895 mji pamoja na ngome zilikodiwa na Uingereza
Waingereza walitumia ngome kama gereza.
Tangu mwaka 1958 imekuwa makumbusho ya kitaifa. Leo hii ni sehemu ya Makumbusho ya Kitaifa ya Kenya na ya urithi wa dunia wa UNESCO.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ngome ya Yesu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.