Nematodi au minyoo-kuru ni faila ya minyoo ambayo ni kati ya faila zenye spishi nyingi katika himaya ya wanyama.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Nematodi
Thumb
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
(bila tabaka): Bilateria
(bila tabaka): Prostomia
Faila ya juu: Ecdysozoa
Faila: Nematoda
Rudolphi, 1808
Ngazi za chini

Ngeli 2

  • Chromadorea
  • Enoplea
Funga

Kutofautisha na kuainisha nematodi ni kazi ngumu. Hadi sasa spishi 80,000 zimeelezwa kitaalamu. Kuna makadirio ya kwamba idadi ya spishi hizo inaweza kufikia nusu milioni. Nematodi wengi ni minyoo midogo myeupe au bila rangi wanayoishi katika mazingira mabichi.

Kati ya nematodi wanaojulikana takriban spishi 15,000 ni za kiparasiti (vimelea) yaani wanaishi ndani ya viumbe wengine. Spishi kadhaa husababisha maradhi mbalimbali ya binadamu. [1]

Mlolongo wa DNA katika uchambuzi wa nematodi umepiga hatua sana, ikiwa ni pamoja na uhusiano na spishi za miti.

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.