Mtumiaji:Kipala/jaribio
From Wikipedia, the free encyclopedia
Msitu ni eneo kubwa penye miti mingi. Misitu inatofautiana kulingana na tabianchi na mazingira hivyo hakuna ufafanuzi kamili msitu uwe na ukubwa gani au idadi gani ya miti. Kwa hiyo haiwezekani kusema kikamilifu tofauti baina ya msitu na kijisitu.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/c/cb/Hellyer_Gorge%2C_Tasmania.jpg/640px-Hellyer_Gorge%2C_Tasmania.jpg)
Siku hizi takriban asilimia 30 za uso wa nchi duniani zimefunikwa kwa misitu; inakadiriwa ya kwamba zamani kulikuwa na nusu ya uso wa nchi duniani iliyokuwa na misitu. Misitu ni muhimu sana kwa ekolojia ya dunia na hivyo kwa uhai wote. Spishi nyingi za viumbehai vinategemea mazingira ya msitu, misitu inadhibiti dura ya maji kuanzia mvua hadi vyanzo vya mito na kulinda ardhi dhidi ya mmomonyoko. Misitu ina umuhimu kwa uchumi wa nchi.