Useja
From Wikipedia, the free encyclopedia
Useja ni hali ya mtu kuishi bila ndoa. Inaweza kutokea kwa sababu mbalimbali, lakini inazingatiwa hasa ile inayotokana na uamuzi kamili wa mhusika asiye na kizuio chochote, hasa kama akichagua kuishi hivyo kwa sababu ya kidini.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/d5/St_Macarius_the_Great_with_Cherub.jpg/200px-St_Macarius_the_Great_with_Cherub.jpg)
Kesi za namna hiyo zimepatikana katika dini karibu zote.
Ni maarufu hasa neno la Yesu katika kutetea wanaofanya hivyo kwa ajili ya Mungu, yeye akiwa mmojawapo (Math 19:11-12).
Katika Ukristo hali ya namna hiyo inaitwa pengine useja mtakatifu na ni msingi wa utawa wa aina yoyote.