From Wikipedia, the free encyclopedia
Mpingakristo katika Biblia ni mtu au watu waliotabiriwa katika Waraka wa kwanza wa Yohane na Waraka wa pili wa Yohane kuwa watatokea kumpinga Yesu Kristo ili kushika nafasi yake[1][2][3].
Badala yake Injili zinawazungumzia Makristo wa uongo[4] na Waraka wa pili kwa Wathesalonike unamtaja "Mtu wa dhambi"[5]
Katika Uislamu, anatajwa Al-Masih ad-Dajjal (المسيح الدجال) kama mmoja atakayetokea kudanganya binadamu kabla ya ujio wa pili wa nabii Isa bin Mariamu (Yesu).
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.