From Wikipedia, the free encyclopedia
Moyo Mtakatifu wa Yesu ni ibada iliyoenea sana, hasa katika Kanisa Katoliki, ikielekea moyo wa Yesu Kristo hasa kama ishara ya upendo wake kwa binadamu[1]. Ibada hiyo inazingatia mateso ya kiroho na ya kimwili ambayo yamethibitisha upendo huo.
Sherehe yake huadhimishwa Ijumaa inayofuata Jumapili ya pili baada ya Pentekoste, kati ya tarehe 29 Mei na 2 Julai[2].
Jinsi ilivyo kwa sasa imetokana hasa na njozi ambazo mmonaki bikira wa Ufaransa Margareta Maria Alacoque alisema amezipata katika miaka 1673 - 1675,[3] Kabla yake katika Karne za Kati watakatifu mbalimbali walipata njozi za namna hiyo, hasa Gertrude Mkuu.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.