![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/sw/thumb/1/1f/Mfumo_mmeng%2527enyo.png/640px-Mfumo_mmeng%2527enyo.png&w=640&q=50)
Mmeng'enyo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mmeng'enyo au umeng'enyaji (en:digestion) ni namna jinsi viumbehai humega chakula kwa pande ndogo zaidi halafu kwa dutu zinazoweza kupokelewa na mwili na kuwa virutubisho vyake.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/sw/thumb/1/1f/Mfumo_mmeng%27enyo.png/640px-Mfumo_mmeng%27enyo.png)
Tasfiri: utumbo Mwembamba (small intestine), utumbo mpana (large intestine), ini (liver), kongosho (pancrease), ulimi (tongue), tumbo (stomach), tezi za mate (salivary glands), umio (esophagus), puru (rectum), mkundu (anus)
Kazi hii inatekelezwa katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Kwa binadamu na wanyama wengi mmengenyo huwa na ngazi mbili
- kusagasaga chakula kwa meno au pande nyingine ili kupata vipande vidogo zaidi
- kumeng'enya vipande vya chakula kwa kemikali za mwilini kama vile vimeng’enya mbalimbali na asidi za tumboni ili kupasua molekuli kubwa kama protini kuwa molekuli ndogo zaidi zinazoweza kutumiwa na mwili kutoa nishati au kama vipande vya kujenga mwili mwenyewe. Utumbo huwa na bakteria nyingi za pekee zinazoshirikiana katika mmeng'enyo.