Mkoa wa Équateur
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mkoa wa Équateur (Mkoa wa Ikweta) ni mmoja ya mikoa 26 ya kujitawala ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Idadi ya wakazi wake ni takriban 1,626,606. Mji mkuu ni Mbandaka.
Mkoa wa Ikweta Ekwatéli / Équateur |
|
![]() Ekwatéli / Équateur |
|
Majiranukta: 00°04′N 18°16′E | |
Nchi | Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |
---|---|
Wilaya | 7 |
Mji mkuu | Mbandaka |
Serikali | |
- Gouverneur | |
Eneo | |
- Jumla | 103,902 km² |
Idadi ya wakazi (1998) | |
- Wakazi kwa ujumla | 1,626,606 |
Mkoa huu ulianzishwa kutokana na ugawaji mpya wa mikoa kadiri ya katiba ya Kongo ya mwaka 2005. Kabla yake ilikuwa sehemu ya jimbo la Equateur pamoja na mikoa ya sasa ya Ubangi-Kaskazini, Mongala, Ubangi-Kusini na Tshuapa. Kabla ya kuingizwa katika jimbo la Equateur wakati wa rais Mobutu Sese Seko uliwahi kuwa mkoa wa pekee kati ya 1962-1966 kwa jina la Cuvette-Centrale.
Eneo la mkoa huu liko katika kaskazini-magharibi ya Kongo kando ya mto Kongo. Upande wa magharibi unapakana na nchi ya Kongo-Brazzaville.
Sehemu kubwa ya Hifadhi ya Taifa ya Lomako Yokokala iko ndani ya mkoa huu. Hifadhi hii inajulikana hasa kwa sababu ndiko mahali pekee duniani wanapoishi nyani kubwa wa Bonobo wanaohesabiwa kati ya hominidi.